Ujumbe kutoka Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro (TIAC), ukiongozwa na Bw. Boniphace Mwabukusi, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Bw. Mpale Mpoki, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TIAC, na Bi. Magreth Magoma, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIAC, umekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Eliakim Maswi, katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, tarehe 14 Agosti 2025.
Ujumbe huo umeishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa kudumisha ushirikiano katika kuendeleza na kuboresha matumizi ya dhana ya Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala.
Aidha, katika kikao hicho, Wizara na TIAC wamekubaliana kuendeleza ushirikiano huo kwa lengo la kuboresha mifumo wezeshi itakayorahisisha upatikanaji wa haki kupitia mfumo wa utatuzi wa migogoro nje ya mahakama. Vilevile, wamejadili umuhimu wa kuwajengea uwezo watoa huduma za usuluhishi ili kuongeza ufanisi katika kutatua migogoro kwa kutumia muda mfupi na gharama nafuu. Hatua hizi zinalenga kuwajengea wawekezaji imani kwa mifumo yetu ya upatikanaji haki, kuimarisha mahusiano, na kuchochea ukuaji wa kiuchumi.
|Tanzania International Arbitration Centre
|Plot No. 391|Chato Street|Regent Estate
|P.O. Box 2148, Dar es Salaam, Tanzania; Tel: +255 772 831 483;
E-mail: info@tiac.or.tz | Follow us on Twitter: |Like us on facebook: |Website www.tiac.or.tz
WE RESPOND TO ALL OFFICIAL EMAILS WITHIN 24 HOURS OF RECEIPT EXCEPT ON WEEKENDS AND PUBLIC HOLIDAYS. IF YOU DO NOT RECEIVE A REPLY TO YOUR EMAIL WITHIN THIS TIME FRAME PLEASE RE-SEND, FAX OR CALL US.
Our Model Arbitration Clause
“Any dispute, controversy or claim arising out of, relating to or in connection with this contract, including any question regarding its existence, validity or termination, shall be resolved by arbitration in accordance with the TANZANIA INTERNATIONAL ARBITRATION CENTRE (TIAC) Arbitration Rules. The seat of arbitration shall be Dar es Salaam, Tanzania [or choose another city]. The language of the arbitration shall be English [or choose another language]. The number of arbitrators shall be one [or three, or delete this sentence and rely on Article 8 of the TANZANIA INTERNATIONAL ARBITRATION CENTRE (TIAC) Arbitration Rules]”.